Timu ya Wanawake ya Mpira wa Pete ya Chuo cha Mipango Jumatano tarehe 15 Novemba , 2023 imeichapa bila huruma timu ya WCF (Workers Compensation Fund) kwa magoli 35 kwa 17 katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma , Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) yanayoendelea Jijini Dodoma.
Mchezo mwingine utachezwa hapo kesho majira ya saa 9:50 Alasiri ambapo timu ya IRDP itakutana na timu ya BOT (Bank Of Tanzania) , mchezo utakaopigwa katika Viwanja vya Kilimani.
Akizungumzia maandalizi na hali ya Kambi kuelekea mchezo huo, Mwalimu wa timu Bw. Mafuru Guriro amesema hali ya Kambi ni nzuri na hakuna majeruhi wowote na kwamba ushindi wa leo umewapa ari kubwa ya kuendelea kushinda.
" Wachezaji wangu wote wana ari kubwa na nitumie fursa hii kuwatumia salamu timu tutakazo kutana nazo wajiandae kisaikolojia. Kwa upande wa BOT wajiandae kupigwa na kitu kizito kichwani ". Alisema Bwana Mafuru