Single Event

Serikali ya Marekani yashirikiana na Chuo cha Mipango kutoa elimu ya ujasiriamali kwa Wanawake.

Serikali ya Marekani kwa kushirikiania na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijiji (IRDP) kupitia mradi wa Academy for Women Entrepreneurs 'AWE' imezindua programu maalum ya kuwafundisha wanawake Ujasiriamali ikiwa ni mchango wa Chuo kwa jamii unaolenga kuwajengea wanawake uwezo wa kupambana na umaskini. "Mradi huu utawawezesha kupata maarifa ya kuanzisha, kusimamia na kuendesha biashara zenu ili kuboresha vipato na kwa kifanya hivyo tutashiriki katika juhudi za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika vita dhidi ya umasikini, Kipanga ni Kuchagua", hayo aliyasema Makamu mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Provident Dimoso wakati wa ufunguzi wa mradi huu leo tarehe 04/04/2022, Mradi huu utatekelezwa kwa wiki kumi na tatu (13) makao makuu ya Chuo cha Mipango Dodoma.