Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini na Viongozi wengine wa Chuo leo Alhamisi tarehe 26/5/2022 wamepata mafunzo ya siku moja juu ya Akili hisia katika Uongozi ( Emotional Intelligence in Leadership) .
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Hoteli ya Nashera Jijini Dodoma. Mwezeshaji katika Semina hiyo alikuwa Dkt. Lusajo Kajula kutoka Taasisi ya Uongozi. Aidha Semina hii itaendelea katika Vikao vijavyo vya Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.