Single Event

MWENGE WA UHURU KUKIMBIZWA HALMASHAURI ZOTE NANE ZA MKOA WA DODOMA - RC DODOMA

Na. Nuru  J. Mangalili

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Staki Senyamule amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika halmashauri zote nane za mkoa wa Dodoma na kuweka mawe ya msingi, kuzindua, na kukagua miradi ya maendeleo. Mh. Senyamule amesema hayo Jumanne tarehe 16 Agosti alipokuwa anapokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh. Peter Serukamba.

Leo umeanza kukimbizwa katika wilaya ya Bahi na kesho utakimbizwa katika Wilaya ya Dodoma Jiji, ambapo Mwenge wa Uhuru utatembelea na kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa barabara Kisasa nyumba 300, kuweka jiwe la msingi mradi wa kitalu nyumba kikundi cha vijana kiu ya ufanisi Viwanja vya nane nane , kuzindua mradi wa Hotel ya Southern Empire na mradi wa Kituo cha Afya cha Chang'ombe.

Ujumbe wa Mwenge  mwaka 2022 ni "Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo Shiriki Kuhesabiwa Tuyafikie Maendeleo ya Taifa".