Timu ya Wanawake ya Mpira wa Pete ya Chuo cha Mipango (IRDP) imepoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Timu ya Bandari (TPA) kwa kufungwa magoli 46 kwa 15 katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) yaliyoanza jana Jumapili tarehe 12 Novemba 2023 Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya Mchezo huo uliochezwa katika Viwanja vya Jamhuri Katibu Mkuu wa Mipango Sports Club Dkt. Swaumu Mkomwa alisema kuwa timu hiyo imepoteza mechi kutokana na kuwa na muda mchache wa kujiandaa na kufanya mazoezi. Hata hivyo ameahidi kuwa timu hiyo itafanya vizuri katika mechi zijazo.
" Niwapongeze wachezaji wangu kwa kucheza vizuri japo hatukupata matokeo mazuri. Ila tunaahidi kufanya vizuri katika mechi zijazo". Alisema Dkt. Swaumu
Ikumbukwe kuwa Timu hiyo ya Bandari ni bingwa mtetezi wa mpira wa Pete wa Mashindano ya Shimmuta mwaka jana 2022.