MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

CHUO CHA MIPANGO CHANYAKUA MAKOMBE MATATU MICHEZO YA SHIMMUTA

  • 2023-12-19 14:20:40

Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini , leo Jumamosi tarehe 25,Novemba,2023 kimenyakua jumla ya Makombe matatu katika Hafla ya Ufungaji wa Mashindano ya SHIMMUTA yaliyokua yakifanyika Jijini Dodoma tangu Novemba 12, 2023.

Makombe hayo ni pamoja na Kombe la Mshindi wa kwanza wa mchezo wa Karata Wanaume ambapo Bwana Magiri Magesa alishinda mchezo huo, Kombe la Pili limetokana na Mbio za Magunia Wanaume ambapo mchezaji Simba Mumwi alicheza mchezo huo na Kombe la tatu la Mchezo wa Draft wanawake Mshindi wa pili ambapo Bi. Sophia Kambaya alishinda mchezo huo.

Mashindano hayo yamefungwa Leo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ambaye alikua Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo.

#TUMETUMWA UBINGWA#

Subcribe weekly newsletter