MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

-

  • 2023-12-19 14:11:31

TUTAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI ZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA - PROF. MAYAYA

Na Mariam Mayunga

Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya amesema Chuo hicho kitaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha na kutunza mazingira hapa nchini.

Hayo yamejiri leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo Chuo cha Mipango kimeadhimisha kwa kupanda miti katika eneo lake la Miyuji Kaskazini.

"Tutaendelea kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais ambaye ni kinara wa utunzaji wa mazingira kwa matumizi ya Nishati safi na salama ya kupikia kwani tumejijengea utamaduni wa kutunza mazingira yetu kwa kupanda miti. Hivyo, ninawaomba watanzania wenzangu tujenge utamaduni wa kupanda miti mara kwa mara" alisema Profesa Mayaya na kuongeza" Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 watanzania tuko zaidi ya milioni sitini. Kama kila mtu atapanda miti miwili kwa mwaka tutakuwa tumepanda miti milioni mia moja na ishirini, Ninatambua kati ya watu hawa milioni sitini wapo na watoto wadogo, hata hivyo familia inawajibu wa kuwapandia miti watoto hawa kwa niaba yao".

Profesa Mayaya amewataka wanajumuiya wa Chuo cha Mipango kuachana na matumizi ya nishati ya mkaa badala yake watumie Nishati rafiki, salama na safi katika shughuli zao za mapishi.

Aidha, ameiasa jamii ya watanzania kuacha tabia ya kukata miti kiholela badala yake waitunze miti hiyo pamoja na visiki hai kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.

''Wakati huo huo Mkuu wa Idara ya Mipango ya Mazingira Profesa Fadhili Mgumia amewataka wanafunzi wanaosoma Idara hiyo kushiriki Maadhimisho ya Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo na Wanafunzi wa mazingira. " Nendeni Kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo yanafanyika Kitaifa katika Ukumbi Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kujifunza asasi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya mazingira."

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Mwaka huu ni ''Urejeshwaji wa ardhi, Ustahimilivu wa hali ya jangwa na ukame''

#Kupanga ni Kuchagua

Subcribe weekly newsletter