MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

News

TUTAENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WETU- PROF. MAYAYA

  • 2023-12-19 11:57:36

Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Prof. Hozen Mayaya alisema Chuo kimeweka kipaumbele katika kuwajengea uwezo watumishi wake katika maeneo mbalimbali ya ubobezi wao ili wapate stadi stahiki katika kuhudumia umma wa watanzania. "Tunaendelea kuwajengea uwezo watumishi wetu katika mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa lengo la kuwa na rasilimali watu mahiri katika kutekeleza majukumu ya ndani ya Chuo na nje" alisema Prof. Mayaya.

Prof Mayaya ameyasema haya jana Alhamisi tarehe 29 Septemba,2022 alipokutana na timu ya wataaalamu wa Chuo wa Masuala ya Uwezeshaji ofisini kwake waliokwenda kuwasilisha mkakati wa kutoa huduma bora kwa jamii.

 Akiwasilisha mkakati huo Makamu Mkuu wa Chuo - Taaluma Prof. Provident Dimoso alisema kwa muda mrefu Chuo kimekuwa na ndoto ya kuwa na kituo cha kuwajengea uwezo wananchi kiuchumi. Ndoto hii ilitimia mwaka 2019 kwa kuanzisha  Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu ( Mipango Entrepreneurship and Innovation ) maarufu MEI . Kwa mujibu wa Prof . Dimoso Kituo hiki tangu kuanzishwa kwake  kimefanya vizuri katika kulea  vipaji vya ubunifu na ujasiriamali kwa wanafunzi wa Chuo cha Mipango. " Mkakati wetu  ni kupanua wigo kwa kuwa na  programu zinazogusa maisha ya jamii kubwa. Vilevile kuendelea na programu ya  kubadilisha mtizamo kwa vijana wetu kuhusu ajira. Msisitizo ni kujiajiri na  kuajiri wengine."alisema Prof. Dimoso na kuongeza, "Ujasiriamali ndio ajenda ya sasa, Vyuo vinazalisha wahitimu wengi  kila mwaka wakati nafasi za ajira ni chache sana hivyo msisitizo na msukumo uwe mkubwa kwenye masuala ya Ujasiriamali na Ubunifu".

Subcribe weekly newsletter