MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

Kikao cha 135 cha Baraza la Uongozi wa Chuo.

  • 2024-02-29 23:47:24

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini CPA. Dkt. Samwel Werema kushoto aliongoza kikao cha 135 cha Baraza la Uongozi wa Chuo leo Alhamisi tarehe 29 Februari 2024.

Pamoja na mambo mengine, kikao kilijadili upandishwaji wa madaraja kwa wahadhiri watano na kuthibitishwa kazini kwa wafanyakazi 22.

Kikao hicho kilitanguliwa na vikao vya Kamati za Baraza la Uongozi wa Chuo cha Ukaguzi tarehe 26 Februari 2024, na tarehe 27 Februari kulifanyika vikao viwili vya Kamati ya Taaluma, na Kamati ya Mipango, Fedha, Utawala na Maendeleo ya Wafanyakazi.

Aidha jana Jumatano tarehe 28 Februari 2024, Wajumbe hao pamoja na viongozi Waandamizi wa Chuo walijengewa uwezo katika masuala ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Mtandao (National e-Procurement System of Tanzania - NeST) pamoja na Usimamizi wa Muda kwenye Vikao (Meeting and Time Management).

#Kupanga ni Kuchagua

Subcribe weekly newsletter