MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

Utekelezaji wa Majukumu kwa Weledi ni Nguzo katika Utumishi wa Umma - Profesa Mayaya

  • 2024-02-20 23:24:18


Na Mariam Mayunga.

Washiriki wa Mafunzo Elekezi kwa Watumishi wapya wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wamekumbushwa kuwa weledi ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Rai hiyo imetolewa leo Jumanne tarehe 20 Februari 2024 na Mkuu wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya katika hafla ya ufunguzi wa Mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa Baraza hapa Chuoni.

"Utekelezaji wa majukumu katika utumishi wa umma unahitaji weledi wa hali ya juu pamoja na uzingatiaji wa sheria , taratibu, na miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali mara kwa mara" alisema Profesa Mayaya na kuongeza " ni matumaini yangu kuwa baada ya mafunzo haya mtakuwa chachu ya mafanikio ya Chuo chetu na Taifa kwa ujumla".

Aidha, amewataka kuwekeza katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wa ndani na nje ya taasisi.

Mafunzo hayo yanayojumuisha watumishi wapya 34 yamezinduliwa leo tarehe 20 Februari 2024 yatahitimishwa Ijumaa tarehe 23 Februari, 2024.

Wawezeshaji wa Mafunzo haya ni Bwana Fadhili Mtinda na Bwana Richard Manase kutoka Chuo Cha Utumishi wa Umma(TPSC - Tabora) na Bw. Salvatory Kilasara kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

#Kupanga ni Kuchagua

Subcribe weekly newsletter