Wadau mbalimbali wameendelea kutembelea Mabanda ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) katika Maonesho ya Nanenane – Kanda ya Kati Nzuguni, Jijini Dodoma na Kanda ya Ziwa Magharibi katika Viwanja vya Nyamhongolo , Manispaaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Wadau hao kutoka sekta mbalimbali wakiwemo wakulima, wajasiriamali, wanafunzi wa vyuo, watendaji wa serikali, na mashirika yasiyo ya kiserikali wamekuwa wakimiminika kwa wingi kujifunza na kupata taarifa muhimu kuhusu mchango wa Chuo katika maendeleo ya nchi kupitia utafiti, huduma za ushauri elelezi, na mafunzo ya muda mfupi.
Aidha, baadhi ya wahitimu wa kidato cha Nne na Kidato cha Sita wameendelea kutumia fursa ya maonesho hayo kutuma maombi ya kujiunga na Chuo kwa njia ya mtandao kupitia oas.irdp.ac.tz , kwa ajili ya kusoma mafunzo ya muda mrefu.
Mabanda haya yataendelea kuwahudumia wadau hadi kufikia kilele cha maonesho hayo Ijumaa Agosti 08, 2025. Yaliyobebwa na kaulimbiu: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi 2025.”