MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

MIPANGO NA CHUO KIKUU CHA ZHEJIANG CHA NCHINI CHINA KUSHIRIKIANA

  • 2024-05-10 11:26:29

Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini pamoja na Chuo Kikuu cha Zhejiang cha nchini China vimeingia makubaliano ya ushirikiano wa kubadilishana uzoefu kwa Wanafunzi na Wanataaluma, kufanya tafiti, kutoa machapisho, na makongamano ya kimataifa kwa pamoja.

Makubaliano hayo yamefanyika Jumatatu Machi 11, 2024 katika hafla ya kutiliana saini hati ya makubariano ya ushirikiano huo iliyofanyika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa - Mwanza.

Katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Afrika ya Chuo Kikuu cha Zhejiang cha nchini China Profesa Liu Hongwe amesema kuwa ushirikiano huo utakuwa na manufaa kwa nchi ya China na Tanzania kwani ushirikiano wa nchi hizi mbili ni wa kihistoria.

“China na Bara la Afrika hususani nchi ya Tanzania tuliwahi kuwa miongoni mwa nchi za dunia ya tatu kiuchumi lakini kwa sasa China imeendelea kwa haraka kiuchumi. Hivyo kupitia makubaliano haya ya ushirikiano wa kubadilishana uzoefu hususani kwa wanataaluma na wanafunzi kutatoa mwanga kwa Tanzania juu ya mabadiliko ya haraka ambayo China imepitia” Alisema Profesa Liu.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa – Mwanza Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Juvenal Nkonoki amesema makubaliano hayo ni fursa kwa Chuo cha Mipango kwani Chuo kinakwenda kunufaika kupitia kubadilishana uzoefu katika programu mbalimbali hususani katika eneo la maendeleo vijijini.

“Hii ni fursa kwa Chuo na taifa kwa ujumla kwani vijana wetu watapata fursa ya kujifunza na kushirikiana siyo tu katika tafiti na machapisho bali pia katika makongamano ya kimataifa na Chuo Kikuu cha Zhejiang ” Alisema Profesa. Nkonoki.

Aliongeza kwa kusema, Chuo kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kilishafanya upembuzi yakinifu katika maeneo mengi ambayo imeibua miradi mingi ya maendeleo vijijini. Changamoto ilikuwa wananchi wengi wanakosa teknolojia bora kwavile wanatumia teknolojia duni katika kilimo, mifugo na uvuvii. Hivyo, ni imani yake ushirikiano huu unakwenda kuibua chachu ya mabadiliko ya teknolojia na mbinu za kutatua changamoto za maendeleo kutoka

Subcribe weekly newsletter