MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

MIPANGO YAJIDHATITI KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA.

  • 2025-06-10 15:33:39

MIPANGO YAJIDHATITI KUTOA ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA.

Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini  kimejipanga kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira  kwa jamii inayowazunguka kwa lengo la kuinusuru jamiii na changamoto za uharibifu wa mazingira. 

Kauli hiyo imetolewa jana na Makamu Mkuu wa Chuo - Mipango, Fedha na Utawala Profesa Canute Hyandye alipotoa hotuba yake kwenye maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani 2025 .   "Kutokana na athari kubwa za taka za plastiki ambazo zinatishia mustakabali wa maisha yetu na ya Tanzania ijayo, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini  tukiwa wadau muhimu wa masuala ya mazingira, tutaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu ya taifa letu na ulimwengu kwa ujumla" alisema na kuongeza " Suala la mazingira linahitaji ushirki wa watu wengi wakiwemo sisi Chuo cha Mipango."

Ili kutekeleza hilo, Mgeni Rasmi alimwelekeza Mkuu wa Idara ya Mipango ya Mazingira Profesa Fadhil Hamza Mgumia kuandaa Mpango wa utoaji elimu ya mazingira kwa jamii inayozunguka Chuo.

Chuo hicho kwa kutambua umuhimu wa masuala ya mazingira kinaendesha kozi za muda mfupi na muda mrefu za masuala ya mazingira. Kozi za muda mrefu katika ngazi ya Shahada, Astahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamili ni pamoja na : Shahada ya kwanza Mipango na Usimamizi wa Mazingira (Bachelor Degree in Environmental Planning and Management); 
Shahada ya kwanza ya Maendeleo ya Miji na Usimaizi wa Mazingira(Bachelor Degree in Urban Development and Environmental Management);
Stashahada ya zamili ya Mipango na Usimamizi wa Mazingira (Post Graduate Diploma in Environmental Planning and Management). Nyingine ni Stashahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Miji na Usimaizi wa Mazingira(Post Graduate Diploma in Urban Development and Environmental Management); na Shahada ya Uzamili ya Afya ya Mazingira na Usimamizi wa Usafi wa Mazingira(Master Degree in Environmental Health and Sanitation Management);

Maadhimisho hayo yaliyofanyika jana, tarehe 4 Juni 2025, chuoni hapo katika eneo la Miyuji Kaskazini (40 Acres), jijini Dodoma, yakiwa na 
kauli mbiu: “Mazingira Yetu na Tanzania Ijayo, Tuwajibike Sasa – Thibiti Matumizi ya Plastiki"' , vijana wa Programu ya Shahada ya Kwanza ya Mazingira waliwasilisha mada juu ya "Plastic Waste Management". Wasilisho hilo lilitanguliwa na upandaji wa miti zaidi ya Mia moja, zoezi lililoongozwa na Mgeni Rasmi Makamu Mkuu wa Chuo - Mipango, Fedha na Utawala Profesa Canute Hyandye. 


Siku ya Mazingira Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Juni. Kwa mwaka huu, maadhimisho ya kitaifa yanatarajiwa kufanyika jijini Dodoma yakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Subcribe weekly newsletter
Apply Now