Event

OFISI YA WAZIRI MKUU NA CHUO CHA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJINI ZASAINI HATI YA MASHIRIKIANO

  • 2026-02-09 15:41:47

OFISI YA WAZIRI MKUU NA CHUO CHA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJINI ZASAINI HATI ZA MASHIRIKIANO

Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) leo tarehe 02 Februari, 2026 zimesaini Hati za Mashirikiano (MoU) kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini. Ushirikiano huo unatarajiwa kuleta mchango mkubwa katika kuimarisha mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmini ya miradi ya maendeleo na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Sera, Mipango, na Programu za Serikali Nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo,  Katibu Mkuu - Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim Yonazi ameeleza umuhimu wa ushirikiano huo katika kuimarisha uwezo wa rasilimali watu katika sekta ya Ufuatiliaji na Tathmini, ambapo utekelezaji wake unazingatia maelekezo ya serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yenye msisitizo wa matokeo yanayopimika na manufaa halisi kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Profesa Hozen Mayaya,  ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuendelea kuipa kipaumbele Sekta ya Ufuatiliaji na Tathmini (Monitoring and Evaluation), akieleza kuwa ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha miradi ya Serikali inaleta tija kwa Wananchi.

Subcribe weekly newsletter
Register Now