Wahitimu tarajali wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa cha Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, wamepatiwa Mafunzo elekezi ya kuwaandaa kukabiliana na soko la ajira nchini .
Mafunzo hayo elekezi yametolewa Jumatatu Januari 19, 2026 na Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano yaliyolenga kuwaandaa Wahitimu hao tarajali kukabiliana na changamoto ya soko la ajira Nchini.
Katika hafla ya kufungua Mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Masula aya Taaluma Dkt. David Ngwilizi kwa niaba ya Mkurugenzi wa wa Kituo ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano kwa kuandaa programu hiyo kwa wahitimu tarajali hapa Nchini.
“Tunawashukuru sana Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mafunzo haya adhimu kwa vijana wetu ambao ni wahitimu tarajali , hakika ni fursa ya kipekee kuwapata wataalamu kama ninyi kwenye kituo chetu. Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo tunaomba mtufikishie shukrani zetu kwa Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi , Ajira na Mahusiano kwa kutupatia programu hii”, alisema. Dkt. Ngwilizi na kuongeza
“Kwa washiriki wa mafunzo ninawaasa kuwawasikivu na kufuatilia kwa karibu mada zote kwani kwa kupitia mafunzo haya mtapata mbinu za namna ya kuomba kazi na hata kujiajiri na hivyo kutengeneza kesho iliyobora”
Mada zilizofundishwa ni pamoja na Mbinu za Kujenga Mtandao wa Mahusiano ya kazi na taaluma; Ujasiliamali na utunzaji wa akiba; Kujiandaa vyema Kitaaluma kwa Ujuzi wa Nadharia na Vitendo; na Kuzingatia Maudhui Mtandaoni.
Register Now