Event

IRDP YAENDELEA KUIMARISHA UMILIKI WA MAENEO YAKE

  • 2026-08-14 17:12:09

Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Profesa Hozen Mayaya (katikati) akipokea  kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala Profesa Canute Hyandye (kushoto) na Afisa Kutoka Miliki Bwana Salumu Bandu (kulia) hati ya eneo la Chuo lililopo Nala, lenye ukubwa wa ekari 645.7.

Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa Mkuu wa Chuo tarehe 10 Agosti, 2026. 

Profesa Mayaya ameipongeza Idara ya Miliki kwa juhudi zake katika kufanikisha mchakato huo, huku akisisitiza kuendelea na mchakato wa kushughulikia hati za maeneo mengine ya Chuo yaliyopo nje ya Dodoma.

Subcribe weekly newsletter
Register Now