MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

Msalato Girls waanzisha Jogging

  • 2024-02-17 10:27:31

Msalato Girls waanzisha Jogging

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Msalato ambayo ni ya vipaji maalumu ya Jijini Dodoma wameanzisha Klabu ya Jogging kwa lengo la kujenga afya zao.

Hatua hiyo imefuatiwa na ziara ya Klabu ya Jogging ya Chuo cha Mipango (Mipango Jogging Club) ilifanyika shuleni hapo kwa lengo la kuhamasisha uanzishaji wa Klabu za Jogging mashuleni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzie Pendo Sheka wa kidato cha sita amesema wamefurahishwa na ujio wa Wanafunzi wa Chuo cha Mipango Kuja kuwahamasisha kuanzisha Klabu ya Jogging.

Aidha, wamevutiwa na kozi mbalimbali za masuala ya mipango zinazotolewa na Chuo cha Mipango na wameahidi kujiunga cha Chuo hicho baada ya kuhitimu masomo yao

#Kupanga ni Kuchagua

Subcribe weekly newsletter