MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

Vikao vya Baraza la Uongozi wa Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.

  • 2024-02-27 07:56:02

Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini CPA. Dkt. Samwel Werema ( kushoto) aliongoza kikao cha 36 cha Kamati ya Ukaguzi ya Baraza la Uongozi wa Chuo jana Jumatatu tarehe 26 Februari 2024.

Pamoja na mambo mengine Kikao kimejadili na kupitisha Mpango kazi wa Mkaguzi wa Ndani.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Vikao vya Baraza Wakili Aisha Mjegele leo Jumanne tarehe 27 Februari 2024 kutafanyika vikao viwili vya Kamati ya Taaluma chini ya Mwenyekiti Dkt. Francis Mwaijande na Kamati ya Mipango, Fedha, Utawala na Maendeleo ya Wafanyakazi chini ya Bw. Benjamini Chilumba.

Kukamilika kwa Vikao hivyo kutatoa fursa ya kufanyika kwa kikao cha 135 cha Baraza la Uongozi wa Chuo siku ya Alhamisi tarehe 29 Februari 2024.

#Kupanga ni Kuchagua

Subcribe weekly newsletter