MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

Mipango Entrepreneurship and Innovation Centre (MEI)

  • 2024-03-13 15:09:29

Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika kikao kazi cha kujadili mpango mkakati wa kituo cha MEI 2024/2025-2028/2029 (Mipango Entrepreneurship and Innovation Centre) kilichofanyika tarehe 28/02/2024 ukumbi wa Baraza hapa Chuoni.
Kikao kazi hicho kilikuwa na lengo la kujadili na kupokea maoni na maboresho ya mpango mkakati wa kituo 2024/2025-2028/2029 kutoka kwa wadau mbalimbali.
Akifungua kikao hicho mkurugenzi wa kurugenzi ya utafiti uelekezi na machapisho Dr. Hosea Mpogole aliwashukuru wadau kwa kuitikia wito na kuwaomba wawe huru kutoa maoni yao ili kuwezesha mpango mkakati huo kukamilika.
Wadau walioshikiriki katika kikao kazi hicho ni pamoja na Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC),Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) , Taasisi ya Twende-Arusha, Alumni wa MEI - IRDP na baadhi ya Wanataaluma kutoka chuo cha Mipango.

 

Subcribe weekly newsletter