MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

TUTAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU NCHINI: - Profesa Nkonoki

  • 2024-05-06 14:20:26

Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa- Mwanza, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Juvenal Nkonoki amesema Chuo kitaendelea kuunga mkono juhudi za serikali na wananchi katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Rai hiyo imetolea Ijumaa Machi 22, 2024 katika hafla ya kukabidhi mabati 156 , misumari Kg 145, na mbao 270 ikiwa ni msaada wa Chuo kwa Shule ya Sekondari ya Mondo iliyopo katika Kijiji cha Kitumba, Kata ya Kisesa Wilayani Magu Mkoani Mwanza.

Akikabidhi msaada huo kwa ajili ya kupaua vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi vyenye thamani ya shilingi milioni kumi laki saba kumi na mbili elfu shuleni hapo mbele ya Uongozi wa Serikali ya Kijiji hicho, Profesa Nkonoki alisema " tukiwa wadau wa elimu nchini tunachukulia kwa uzito wa juu suala la uwekezaji kwenye sekta ya elimu. Hivyo, kwa niaba ya uongozi wa Chuo tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kuchangia katika maeneo tofauti tofauti kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu kwa minajiri ya kuboresha sekta hii muhimu katika jamii” Alisema Profesa Nkonoki.

Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa Kijiji cha Kitumba Bwana Malale Kihila ameushukuru uongozi wa Chuo cha Mipango kwa msaada huo ambao amesema utasaidia kupunguza changamoto waliyokuwa wakikabiliana nayo ya uhaba wa vyumba vya madarasa . “Tunaushukuru sana uongozi wa Chuo kwa haya yanayofanyika katika Kijiji chetu. Ushirikiano huu haujaanza leo tangu. Tangu Kituo kilipohamia mahali hapa mmekuwa msaada mkubwa kwa Kijiji chetu katika huduma za jamii ikiwemo elimu na afya” Alisema Bw. Kihila.

Subcribe weekly newsletter