MINISTRY OF FINANCE

INSTITUTE OF RURAL DEVELOPMENT PLANNING

Kupanga ni Kuchagua

Event

NAWAPONGEZA KWA USHINDI WA KISHINDO MEI MOSI TAIFA 2024 - PROFESA MAYAYA

  • 2024-05-16 15:47:11


Na Mariam Mayunga

Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini amewapongeza Wanamichezo wote kwa Kunyakua makombe mawili ya mshindi wa kwanza kwenye Mashindano ya Mei mosi Taifa Jijini Arusha,

Haya ameyasema leo kwenye kikao cha Menejimenti akikabidhiwa Vikombe vya Mei mosi kutoka kwa wachezaji walioshiriki michezo ya MEI MOSI Jijini Arusha kuanzia tarehe 16/04/2024 hadi 29/04/2024.

''Ninawapongeza kwa Ushindi mlioupata, hakika Mmeupiga mwingi na Mmeiletea heshima kubwa Taasisi yetu. Ninawaahidi kuwa Uongozi wa Chuo utaendelea kutilia mkazo katika suala zima la Michezo kwani michezo inatengeneza mtandao wa kufahamiana na watu na kuboresha afya ya akili.''

Akiongea baada ya kukabidhi Vikombe hivyo, Katibu wa Mipango sport Club Dkt. Swaumu Mkomwa alisema katika michezo hiyo Chuo kilishinda Vikombe Viwili katika mchezo wa Bao (wanawake) na Drafti wanawake.

"Kwa niaba ya Wanamichezo wenzangu naushukuru sana Uongozi wa Chuo kutuwezesha kushiriki mashindano hayo."

Chuo cha Mipango ni miongoni mwa Taasisi 56 zilizoshiriki katika Mashindano hayo ya Mei mosi kitaifa.

Kupanga ni Kuchagua#

Subcribe weekly newsletter