Wanataaluma wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa wamefanya kikao cha mapitio ya Sera ya Upandaji wa Madaraja kwa Wanataaluma ya Mwaka 2022 leo Jumatatu tarehe 15 Desemba 2025, ili iendane na maelekezo ya Utumishi kuhusu “Harmonized Scheme of Service” pamoja na mabadiliko mengine.
Katika kikao hicho, manufaa ya upandaji madaraja yameelezwa kuwa ni pamoja na kuwapa wanataaluma fursa ya kufundisha katika vyuo vilivyopo ndani ya Afrika Mashariki, pamoja na kuweka ‘Uwazi na Usawa’ katika mchakato wa upandaji madaraja kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.
Akizungumza katika kikao hicho, muwezeshaji Profesa Innocent Zilihoma alisema “Kupanda mpaka kuwa Profesa ni tunda la mchakato lakini swali kuu ni kuwa utafanya nini na hiyo ‘title’? Lazima ufanye kazi zinazoonekana ndani na nje ya Chuo pamoja na kuwasaidia wanataaluma wachanga katika kuwashirikisha kwenye uandishi wa machapisho na mambo yanaendana na hayo”.
Inatarajiwa kuwa maboresho ya sera hiyo yataleta chachu ya uwajibikaji, maendeleo ya taaluma na mchango chanya kwa jamii.
Register Now